Ukumbi Wa Mashairi

Rabbi Mola Mswifika


                        Muumba na kuumbuwa
                        swifazo mekamilika,
                        hakuna lilopunguwa 
                        Rabbi nondosha wahaka
                        mahaba yataniuwa,

SIJIFANYIZE MGUMBA

Salamu zifike kwawe, mjini unayetamba,
Hebu ondowa kiwewe, jikanye unayolumba,
Kweli wacha uambiwe, sijifanyize mshamba,
Sijfanyize mgumba,kuteta na walozaa.

Nyuki kuunda asali, bungo huunda udongo.

Tofauti taamuli, kilichoko kwenye bongo, 
Ninazo zangu akili, unayo yako mipango, 
Huluka ni mbalimbali, sio wote wa maringo, 
Nyuki kuunda asali, bungo huunda udongo.

NAOMBA YAKE MAJIBU

Maajabu duniani.....Yaushangaza mtima
Maajabu ya kunguni.......Kutaka jembe kulima
Keshachoka kwa ndani.......Njaa inamsakama
MAAJABU MAAJABU.....NAOMBA YAKE MAJIBU