Hebu ondowa kiwewe, jikanye unayolumba,
Kweli wacha uambiwe, sijifanyize mshamba,
Sijfanyize mgumba,kuteta na walozaa.
Wataka useme wewe, wengineo kuwafumba,
Asemapo mwenginewe, ufunganyishe vilemba,
Atakuwa mkosawe, achaguwe cha kuimba,
Sijifanyize mgumba, kuteta na walozaa.
Mpiga ngoma ni wewe, na ndiwe mwenye kuimba,
Hutaki iingiliwe,isifanyiwe halamba,
Ya wenzio ukaguwe,uwataje ni makomba,
Sijifanyize mgumba, kuteta na walozaa.
Wataka uogopewe, na wasovaa vilemba,
Katu hutii kiwewe, hatuchi hatutosumba,
Akuogopaye wewe, ni ulomwacha na mimba,
Sijifanyize mgumba, kuteta na walozaa.
Tamati twakwambiawe,kama hutaki kulumba,
Jikwamishe huko wewe, huku kwetu tutalumba,
Hutaki tukukosowe,kikosolewa wavimba,
Sijifanyize mgumba, kuteta na walozaa.
No comments:
Post a Comment